May 15, 2016


Daktari wa klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini, amemzuia mshambuliaji Mtanzania Mrisho Ngassa kurejea uwanjani.

Daktari amemtaka Ngassa kuendelea na mazoezi ya gym akiwa na hofu kama ataingia uwanjani anaweza kutonesha goti.

Ngassa alifanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini hivi karibuni.

Akizungumza na Salehjembe kutoka Afrika Kusini, Ngassa amesema, daktari amemshauri kufanya hivyo.

“Aliona mechi zimeisha na msimu unaisha, zilikuwa zimebaki kama mechi tatu hivi. Sasa imebaki mechi moja tu.

“Hivyo aliona bora niendelee na mazoezi ya gym huku nikisubiri msimu ujao. Msimu huu ndiyo umeisha hivyo,” alisema Ngassa.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV