May 8, 2016


Mchezaji Ritchie De Laet alilazimika kuendesha gari lake fasta kwenda Uwanja wa Riverside kuchukua medali yake ya ubingwa wa Ligi Kuu England.

Dae Laet alikuwa tayari amepokea medali ya nafasi ya pili ya ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza England akiwa na Middlesbrough.

Hivyo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyevaa medali mbili za Ligi Kuu England na Ligi Daraja la Kwanza England, siku moja.

Kwanini baada ya kukabidhiwa medali ya daraja la kwanza akaifuata ya ligi kuu?


Dae Laet ni mchezaji wa Leicester City, alipelekwa kucheza kwa mkopo Middlesbrough ambayo ikashika nafasi ya pili na kupanda daraja hadi ligi kuu.

Lakini Leicester ambayo ni timu yake hasa, ikabeba ubingwa wa Ligi Kuu England, naye anahesabika pia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV