May 23, 2016Wachezaji wa Manchester United wameonyesha hofu katakana na taarifa za ujio wa kocha Jose Mourinho anayeelezwa anatarajia kuchukua mikoba ya Louis van Gaal.

The Special One ndiye gumzo, kwamba atachukua mikoba ya van Gaal licha ya kocha huyo kuiwezesha Man United kubeba Kombe la FA.

Taarifa kutoka ndani ya Manchester United kupitia Sportsmail zimeeleza wachezaji wakongwe wa Man United wanaonyesha kutofurahishwa na hilo.

Huenda ni hofu ya kupoteza ajira, kwa kuwa wanaamini iwapo Mreno huyo atapata nafasi, lazima atafanya mabadiliko makubwa.

Hofu yao nyingine ni kwamba, Mourinho hawezi kwenda na mfumo kama wa van Gaal, hivyo atabadili mambo mengi na kuwachanganya.


Imeelezwa uongozi wa Man United, ulitoa pauni million 4 na kumpa Mourinho ili asijiunge na timu nyingine kusubiri waachane na van Gaal na kumchukua yeye.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV