Pamoja na kumaliza msimu akiwa nje, mshambuliaji wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Ngassa ameendelea kujifua gym.
Ngassa alilazimika kumaliza msimu akiwa nje baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
“Nimekuwa nikiendelea na mazoezi kama kawaida, hii ni kutaka kuwa fiti zaidi,” alisema Ngassa.
Awali, Ngassa alikuwa amejipatia namba katika kikosi cha kwanza, lakini upasuaji huo ulimuweka nje na hata baada ya kupona, daktari alimzuia kurejea uwanjani akisisitiza tayari ligi ilikuwa imeisha na angeweza kuendelea na mazoezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment