May 3, 2016


Kikosi cha Yanga kipo tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Stand United ya mjini Shinyanga.

Yanga itakuwa mgeni wa Stand United katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga, leo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema wanajua ugumu wa kila mechi kati ya zilizobaki na hii ya leo dhidi ya Stand United ni mojawapo.

Pluijm amesema anatambua Stand United ni timu bora, hivyo watacheza kwa tahadhari kubwa.

“Lazima tuwe makini, wachezaji walifanya kazi kubwa katika mechi iliyopita dhidi ya Toto African.

“Wanajua kwamba ni kazi nyingine ngumu dhidi ya Stand,” alisema Pluijm.

Tayari Yanga wako mjini Shinyanga ambako wamekuwa wakifanya maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa.

Yanga ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara na ushindi wa mechi ya leo utawapeleka karibu kabisa na ubingwa. Lakini kama watapoteza, wataanzisha hofu kwa kuwa Azam FC, bado wanaonekana kuwa na nguvu kuendelea kupambana wakiutaka ubingwa.

2 COMMENTS:

  1. All the best my lovely team(YANGA).

    ReplyDelete
    Replies
    1. Let us pray for them.

      Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV