June 10, 2016

MAYANJA
Baada ya Simba kugonga mwamba kumnyakua kocha wa timu ya taifa ya Zimbabwe, Kalisto Pasuwa sasa imeamua kugeukia nchini Ghana kutafuta bosi mpya wa benchi la ufundi la timu hiyo.

Kwa sasa kikosi cha Simba kipo chini ya Kocha Jackson Mayanja raia wa Uganda ambaye ni msaidizi.

Awali Simba ilisafiri mpaka nchini Zimbabwe kwenda kuzungumza na Pasuwa lakini kila kitu kiliharibika baada ya kocha huyo kuiwezesha Zimbabwe kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), akionekana bado anahitaji kuiongoza timu hiyo katika michuano hiyo huko Gabon mwakani.

Hali hiyo imesababisha Simba kuanza mazungumzo ya siri na kocha mwingine kutoka Ghana ambaye hajafahamika jina mara moja wala timu anayofundisha kwa sasa ikidaiwa imekuwa hivyo kwa kuwa Wekundu hao wanataka kumaliza mambo kimyakimya.

“Kulikuwa na yule kocha wa Senegal na hata Joseph Omog (Mcameroon) naye alifikiriwa lakini sasa hivi kuna kocha kutoka Ghana ndiye tupo kwenye mazungumzo naye na mambo yakienda vizuri anaweza kuwa nasi msimu ujao,” alisema kigogo mmoja kutoka Simba.

Tangu Simba ilipomfukuza kocha wake Muingereza, Dylan Kerr msimu uliopita, kwa muda mrefu sasa imekuwa ikisaka kocha mpya atakayekuja kusaidiana na Mganda, Jackson Mayanja.

Tayari Simba imekuwa ikihusishwa kumuhitaji Mskochi, Bobby Williamson huku makocha wao wengine wa zamani kama Waserbia, Goran Kopunovic na Milovan Cirkovic wakiwasilisha maombi ya kurejea kukinoa kikosi hicho.

Lakini taarifa nyingine zinaeleza kuwa Simba imewafungia vioo makocha wa kizungu na sasa inahitaji Waafrika wanaolielewa hasa soka la ukanda wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kuja kuinyanyua timu hiyo.


Alipoulizwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema:”Mimi naumwa na sina taarifa yoyote kwa sasa."

SOURCE: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Kweli wewe Saleh ni kubwa jinga,uliandika hapa kuwa Simba yamalizana na kocha wa akina Ngoma sasa leo tena unabadilika kama kinyonga!kweli nimeamini kuwa kila anayeshabikia Simba akili yake inafanana na Kaburu!

    ReplyDelete
  2. Simba SC inaitaji ipate cocha mwenye kulifahamu soka LA Africa mashariki vzr pmj na mpira WA kiafrica Ulivyo Je? Kocha mwenye sifa izo ni Nani Hakuna zaidi Ya Bobby Williamson Alokua akiifundisha team ya taifa ya Uganda ipate namba sita mzuri km Hassan waswa ni sehemu ndogo tu za kurekebisha ili team iwe vzr kwenye ushindani

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV