June 16, 2016


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema klabu hiyo imekuwa ikiendelea kufanya usajili wake kwa hatua na raha kwa kuwa haina sababu ya kugombea chochote na Yanga au timu nyingine.

Hans Poppe ameiambia SALEHJEMBE kwamba Simba inajua inachokifanya na imekuwa ikifanya usajili wake bila ya bugudha yoyote.

“Kama kuna mchezaji Yanga inataka kumchukua, sisi hatukuwa tumemlenga. Hatukuwa na sababu ya kutaka mchezaji yoyote ambaye wao pia walimtaka.

“Simba tuna mipango yetu, pia Yanga wana mipango yao kama ilivyo kwa Azam na timu nyingine. Sisi tunaendelea vizuri na hakuna ambacho kimetushinda hadi sasa,” alisema Hans Poppe.Alisisitiza Simba imekuwa ikiendelea na mazungumzo na wachezaji wengine wa ndani na nje kwa mujibu wa ripoti ya kocha na nini walichokuwa wanakihitaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV