June 20, 2016


Straika wa Yanga, Malimi Busungu, ambaye alikuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha ya mbavu aliyoyapata kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Sagrada Esparanca, ameanza mazoezi mepesi.

Busungu alivunjika mbavu kwenye mchezo huo uliopigwa Mei 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo ilimlazimu kukosa michezo kadhaa ya timu hiyo. 

Akizungumza, kiungo huyo aliyejiunga na Yanga msimu uliomalizika hivi karibuni akitokea Mgambo JKT, alisema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri na ameshaanza mazoezi mepesi kabla ya kujiunga na wenzake kwa ajili ya mazoezi ya pamoja.

“Mwanzo nilikatazwa kabisa kufanya mazoezi lakini kwa sasa hali imeendelea vizuri ambapo nimeambiwa nianze mazoezi mepesi na nimeshaanza kabla ya kujiunga na timu kwa ajili ya mazoezi ya pamoja.

“Katika siku mbili tatu hizi nitafanya ‘check up’ ili kuona hali inaendeleaje, kama majibu yataonyesha naendelea vizuri basi nitarudi kikosini, ila kifupi kwa sasa naendelea vizuri na ‘soon’ nitarudi kwenye timu, nipo chini ya uangalizi wa madaktari makini, hivyo sina wasiwasi wa kupona haraka,” alisema Busungu. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV