June 20, 2016Wakati pazia la usajili likiwa limefunguliwa juzi Jumatano, uongozi wa Azam umetamka hadharani kuwa hautakuwa na muda wa kufanya usajili wa ndani kama ambavyo wamekuwa wakifanya na badala yake watajikita katika kuibua vipaji vya wachezaji wao vijana kutoka kikosi B kwa ajili ya kuwapa uzoefu.

Kwa kipindi kirefu Azam imekuwa ikifanya usajili wa wachezaji ambao tayari wana uzoefu na ligi kuu ambapo msimu uliopita waliwanasa Ramadhan Singano ‘Messi’ kutoka Simba na Ame Ali ‘Zungu’ kutoka Mtibwa.

Msemaji wa Azam, Jaffar Idd, amesema kuwa maamuzi hayo yameamuliwa na viongozi wa timu hiyo baada ya kuona kuwa wachezaji hao hawana msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho kutokana na wengi kucheza bila ya mapenzi.

 “Kwa msimu huu tumeazimia kutofanya usajili wa wachezaji wa ndani, badala yake tutajikita zaidi katika kupandisha wachezaji kutoka kikosi B ambao tumeona sasa ni muda wao muafaka kuwatangaza.

“Maamuzi hayo yamekuja baada ya kuona kuwa hawa tunaowasajili mara nyingi wamekuwa wakicheza bila kujituma kuipigania timu na mwishowe tunakuja kuwaacha tu,” alisema Jaffar.   


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV