June 20, 2016


Sasa ni siku chache tu baada ya Yanga kufanikiwa kumsajili, Obrey Chirwa raia wa Zambia, mpachika mabao wa timu hiyo, raia wa Burundi, Amissi Tambwe, amedai kuwa hana wasiwasi na ujio wa nyota huyo kikosini hapo.

Yanga imemleta Chirwa kutoka FC Platinum ya Zimbabwe ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita baada ya kupiga mabao 21, amesema anajiamini na ana uhakika wa kubakia katika kikosi cha kwanza cha Yanga endapo kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm atapenda.

“Sina wasiwasi na nafasi yangu kwani najiamini na Mungu akipenda nitaendelea kuwa kikosi cha kwanza na nitazidi kufanya vizuri kama ilivyokuwa msimu uliopita.

“Naongea hivyo kwa sababu najiamini na ninajua nini ninachokifanya, kwa hiyo sihofii mchezaji yeyote ila nawapongeza Yanga kwa usajili wa Chirwa kwani tunachotaka sisi ni mafanikio, hivyo nitashirikiana naye kwa kila jambo kama nilivyokuwa nikishirikiana na (Donald) Ngoma,” alisema Tambwe.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV