June 30, 2016


Kiungo wa pembeni wa zamani wa Simba, Haruna Chanongo ni kati ya wachezaji waliotangazwa kutemwa katika kikosi cha Stand United.

Chanongo ametemwa miezi michache baada ya kupata nafasi ya kufanya majaribio TP Mazembe ya DR Congo ambao ni vigogo na mabingwa wa Afrika.

Chanongo ametemwa siku chache baada ya juhudi zake za kutaka kurejea Simba kukwama!

Lakini, Chanongo aliyeondoka Simba kwa tuhuma za utovu wa nidhamu, ametemwa Stand baada ya kuweka rekodi ya kukataliwa na Yanga, Azam FC kumtangaza kuwa haimhitaji baada ya kuonekana na jezi yake mtandaoni.


Pamoja naye, wengine wametemwa ni beki wa zamani wa Yanga, Abuu Ubwa, Nassor Masoud ‘Cholo’, Phillip Metusela na Hassan Banda. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV