June 30, 2016


Si unamjua Ryan Giggs? Ameamua kuondoka Manchester United baada ya kuitumikia kwa miaka 29 akiwa mchezaji na kocha msaidizi.

Giggs anaondoka baada ya kukataa ofa ya kuwa kocha msaidizi chini ya Kocha Mpya, Jose Mourinho.


Kabla, amekuwa kocha msaidizi chini ya makocha wawili David Moyes na Louis van Gaal ambaye alifanikiwa kubeba Kombe la FA.

Giggs ,44, alijiunga Man United mwaka 1987 akiwa ndiyo anasherekea siku yake ya kuzaliwa wakati akitimiza miaka 14. Alitokea timu ya watoto ya Manchester City.DAILY MAIL

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV