June 22, 2016

CHIRWA
Mshambuliaji Obey Chirwa, amekwea pipa kwenda nchini Uturuki kuungana na kikosi cha Yanga kilichoweka kambi nchini Uturuki.

CHIRWA AKIWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (JNIA), TAYARI KWA SAFARI HIYO. AKIWA NA MKUU WA KITENGE CHA HABARI NA MAWASILIANO CHA YANGA, JERRY MURO.

Chirwa raia wa Zambia aliyejiunga na Yanga akitokea FC Platinums ya Zimbabwe anatarajia kuanza mara moja mazoezi baada ya kutua nchini humo ili kuchukua nafasi ya Tambwe.

Atachukua nafasi ya Tambwe katika mechi dhidi ya TP Mazembe kwa kuwa mshambuliaji huyo raia wa Burundi ana kadi mbili za njano zitazomzuia kucheza mechi hiyo.

Chirwa ameonekana akiwa ni mwenye furaha wakati alipokuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), tayari kwa safari hiyo ya Uturuki.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV