June 28, 2016


Mageti ya kuingilia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar res Salaam kwa kuwa mashabiki wameingia na hakuna nafasi.

Baadhi ya mashabiki walifika usiku na kulala nje ya uwanja wa taifa na wengine walifika hapo tokea alfajiri.

Lakini hadi kufikia saa 6 na dakika 14 mchana, tayari Jeshi la Polisi Tanzania waliamuru kufungwa kwa mageti kwa ajili ya masuala ya usalama.

Jeshi la Polisi Tanzania limetoa vijana 500 kuhudhuria mechi ya ya Yanga dhidi ya TP Mazembe ambayo tayari mashabiki wameingia uwanjani kwa wingi kwelikweli.

Idadi ya watu imekuwa juu kwa kuwa hakuna kiingilio na Jeshi la Polisi Tanzania limesisitiza suala la amani na utulivu.


Mashabiki wametakiwa kuingia kwa amani, washuhudie mechi hiyo na warejee nyumbani kwa amani

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV