June 28, 2016


Jeshi la Polisi Tanzania limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki wanaotaka kuingia kwenye Uwanja wa Taifa licha ya kwamba hakuna nafasi.

Tayari mageti yamefungwa, lakini mashabiki walitaka kuingia zaidi ya hapo licha ya maelekezo ya polisi.

Baada ya kutangaziwa wanatakiwa kurejea nyumbani, mashabiki hao walionekana kugoma, mwisho walitakiwa kuondoka kwa kutumia mabomu ya machozi.

Jeshi la Polisi limetoa vijana 500 kuhudhuria mechi ya ya Yanga dhidi ya TP Mazembe ambayo tayari mashabiki wameingia uwanjani kwa wingi kwelikweli.


Idadi ya watu imekuwa juu kwa kuwa hakuna kiingilio na Jeshi la Polisi Tanzania limesisitiza suala la amani na utulivu.

2 COMMENTS:

 1. hii paragraph wala sijailewa

  Jeshi la Polisi limetoa vijana 500 kuhudhuria mechi ya ya Yanga dhidi ya TP Mazembe ambayo tayari mashabiki wameingia uwanjani kwa wingi kwelikweli.

  Na si mara kwanza salehe unaandika para hazieleweki nini zinazungumzi. tafadhari tunaomba uwe makini unapoandika, ni vizuri ukapatia maandishi yako kabla hujayapeleka hewani

  ReplyDelete
  Replies
  1. ASKARI 500 WATAKUWA UWANJANI KWA AJILI YA ULINZI

   Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV