June 19, 2016


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ametupa dongo na kusema wazi kwamba anaiombea Yanga dua mbaya.

Hans Poppe ametumia msemo wa adui muombee njaa huku akisema kwamba anataka Yanga itandikwe hata mabao saba katika mechi yake ya Kombe la Shirikisho leo dhidi ya Mo Bejaia inayopigwa kwenye mji wa Bejaia nchini Algeria, saa chache zijazo.

“Kweli wafungwe tu, mimi niko wazi kwamba siwezi kuiombea Yanga dua nzuri. Wao wamekuwa wakiimba sana kuhusiana na Simba, waliwahi kusema uzalendo umewashinda.

“Sipendi kuwa mnafiki, wafungwe tu na hicho ndicho ninaamini shabiki yoyote wa Simba mwenye malengo anaweza kuwaza,” alisema Hans Poppe akisisitiza, Yanga wakifungwa, kwao ni furaha.


Alipoulizwa kuhusiana na suala la uzalendo: “Sasa Yanga ni timu ya taifa? Uzalendo upi sasa? Wafungwe tu na huko Uarabuni ndiyo kwenye tano, saba.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV