June 19, 2016


KALABA
TP Mazembe imeanza hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kwa kishindo baada ya kutoa kipigo cha mabao 3-1 kwa wageni wake, Medeama kutoka Ghana.

Medeama wamekutana na adhabu hiyo mjini Lubumbashi, DR Congo ikiwa ni mechi ya kwanza kabisa ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.

Medema ndiyo walitangulia kupata bao kupitia Malik Okowuah katika dakika ya nne tu ya mchezo. Hali hiyo ilionekana kuwazindua Mazembe ambao wakaanza kushambulia mfululizo.

Rainford Kalaba ndiye alianza kutikisa nyavu za Medeama katika dakika ya 21 kabya ya Salif Coulibaly kuandika bao la pili katika dakika ya 45. Timu hizo zikaenda mapumziko wenyeji wakiwa wanaongoza kwa idadi hiyo.


Kipindi cha pili kilionekana cha Mazembe wakitawala kila idara hadi Kalaba alipofunga bao la tatu katika dakika ya 73.

Mazembe na Medeama ziko kundi A ambalo wawakilishi wa Tanzania, Yanga pia wamo na wanatarajia kucheza dhidi ya Mo Bejaia wakiwa ugenini katika mechi inayosubiriwa kwa hamu saa chache zijazo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV