June 28, 2016
Wengi walitaka kujua kama Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe kama atakuwepo uwanjani, leo.

Yanga inaivaa TP Mazembe katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ses Salaam na uongozi wa Yanga kupitia mwenyekiti wake, Yusuf Manji umefuta kiingilio.

Hans Poppe amezungumza na SALEHJEMBE na kusema, kamwe hawezi kwenda uwanjani.

Sababu mbili, zitamfanya Hans Poppe asiende uwanjani.

SABABU YA KWANZA:
"Kawaida mimi nakwenda uwanjani kuangalia mechi za Simba, sijawahi kuona mechi ya Yanga hata moja. Kama nimewahi kuwaona wanacheza nikiwa uwanjani basi ni dhidi ya Simba tu."

SABABU YA PILI:
"Uzalendo kwani Yanga ni timu ya taifa, kama ni kuona Mazembe wanavyochezam nitaangalia kwenye TV."

Tayari Jeshi la Polisi Tanzania limetoa vijana 500 kuhudhuria mechi ya ya Yanga dhidi ya TP Mazembe ambayo tayari mashabiki wameingia uwanjani kwa wingi kwelikweli na tayari mageti yaishafungwa na walio nje wametakiwa kurejea nyumbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV