June 3, 2016

JEBA (KULIA)...
Uongozi wa Mtibwa Sugar umeionya Klabu ya Simba kuwa makini na suala la kuwazungumzia au kufanya mazungumzo na wachezaji wake ambao wana mikataba nao.

Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser amesema amekuwa akisikia Simba ina mpango wa kuwasajili wachezaji watatu Shiza Kichuya, Ibrahim Rajab ‘Jeba’ na Ally Shomari. Lakini wana mkataba na Simba wanapaswa kuheshimu hilo.

“Kama watakuwa wanazungumza wajue wanavunja kanuni na si sahihi, wakae nao mbali na kama wanavutiwa nao basi waje tuzungumze nao,” alisema.

“Nimekuwa nikisikia tu kwenye vyombo vya habari, niseme tu kuwa nawakaribisha Simba waje.”
Kumekuwa na taarifa kwamba Simba ina mpango wa kuwasajili wachezaji hao katika harakati za kuimarisha kikosi chake.

Simba iko katika mikakati ya kuimarisha kikosi chake kuhakikisha inarejea katika heshima yake ikiwemo kushiriki michuano ya kimataifa.


1 COMMENTS:

  1. Hilo ni lile zee linalovaa kofia ya cowboy,yaani lina shida ajabu!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV