June 29, 2016Baada ya kusubiriwa kwa muda mwingi, hatimaye Manchester United inatarajia kumtangaza rasmi Zlatan Ibrahimovic kuwa mchezaji wake mpya.

Zlatan,34, atatangazwa Ijumaa hii kuwa mchezaji wa Man United iliyo chini ya Jose Mourinho.

Raia huyo wa Sweden amemaliza mkataba wake na PSG ya Ufaransa ambako alifanya vema baada ya maisha yake ya soka akiwa Ajax nchini Uholanzi baadaye nchini Italia akiwa na Juventus, Inter Milan na AC Milan, pia Barcelona ya Hispania.

Taarifa zinaeleza kwamba Man United na Zlatan kila kitu kipo katika hatua za mwisho kabisa.

DAILY MAILY

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV