June 29, 2016

KALI WAKATI AKIKIPIGA AZAM FC...

Aliyekuwa kocha msaidizi wa Azam, Kally Ongala, amepewa ofa ya mwaka mmoja ya kuendelea kukinoa kikosi cha Majimaji baada ya mkataba wa awali kumalizika hivi karibuni.

Ongala alikuwa kocha msaidizi wa Azam na alitangaza kujiondoa kikosini hapo Novemba, 2014 huku akisema anakwenda Uingereza kusomea ukocha ngazi ya juu zaidi kabla ya kurejea nchini na kujiunga na Majimaji Januari, mwaka huu.

Meneja wa Majimaji, God Mvula, amesema: “Tumefanikiwa kumbakisha kocha wetu Ongala na tutaendelea kuwa naye kwa msimu mzima ujao kwani mkataba wake ni wa mwaka mmoja.

“Baada ya kumalizana naye, sasa tupo kwenye mchakato wa kuona ni namna gani tunajenga kikosi chetu kipya kwa ajili ya msimu ujao ambapo usajili wetu tutazingatia kile alichowasilisha kwenye ripoti yake.”

Ongala alikabidhiwa kikosi cha Majimaji kikiwa kinaburuza mkia na pointi 11 baada ya kucheza mechi 13, lakini akapigana na kufanikiwa kumaliza ligi nafasi ya kumi baada ya kujikusanyia pointi 35.


Kwa kipindi alichokabidhiwa timu, Ongala alifanikiwa kuiongoza katika mechi 17 na kukusanya pointi 24, ambazo ziliwaokoa na hatari ya kushuka daraja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV