June 27, 2016

Kuelekea katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa kesho Jumanne saa 10:00 jioni, uongozi wa Klabu ya Yanga umesema kuwa wanatarajia kuwapokea zaidi ya mashabiki mia tano wa TP Mazembe ambao watakuwepo uwanjani kuishangilia timu yao. 




     Licha ya Yanga kutangaza kuwa mchezo huo  utakuwa ni bure ambapo unatarajia kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro amesema tayari wameshapokea tarifa kutoka kwa wapinzani wao hao kuwa watakuwa na mashabiki zaidi ya mia tano kutoka nchini DR Congo kwa ajili ya kuisapoti timu yao.

“Tumepokea taarifa kutoka kwa wenzetu wa TP Mazembe ambao wametueleza kuwa kuna msafara mashabiki wao wapatao mia tano wapo njiani, wanakuja kwa ajili ya kuisapoti timu yao katika mchezo wa kesho,” alisema Muro na kuongeza:
     “Sasa niwaombe tu mashabiki wa Yanga na Watanzania kwa jumla wajitokeze kwa wingi   uwanjani ili tuwazidi hao wa kwao mia tano.”

Mashabiki wa TP Mazembe wanajulikana kwa kuwa na nguvu kubwa ya kushangilia bila kujali wakiwa nyumbani au ugenini, ambapo walipowahi kuja nchini miaka kadhaa iliyopita kucheza dhidi ya Simba walikuwa na kikundi cha ngoma kilichokuwa kivutio kwa mashabiki wengi nchini. 




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic