June 27, 2016

Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) imetangaza kuwa imeachana na aliyekuwa kocha wake, Laurent Blanc ambaye amedumu klabuni hapo katika nafasi hiyo kwa miaka mitatu.

 


Kuondoka kwa Blac, beki wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, kunampa nafasi kocha wa zamani wa Sevilla, Unai Emery ambaye ndiye anayetarajiwa kuchukua nafasi hiyo.

Blanc aliteuliwa kuwa kocha wa PSG mwaka 2013 na kuingozia timu hiyo kutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligue 1, makombe mawili ya Coupe de France na ubingwa mara tatu wa kombe la Coupe de la Ligue.

Kuondoka kwake kunakuja baada ya Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi kunukuliwa akitoa kauli wiki chache zilizopita kuwa kutakuwa na mchakato wa kukijenga upya kikosi cha timu yao .  


Blanc  ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo, Februari mwaka huu, anatarajiwa kulipwa euro milioni 22 ikiwa ni fidia ya kuvunjwa kwa mkataba wake.
  Kuondoka kwa Blac kumekuja ikiwa ni siku chache pia tangu klabu hiyo ilipomruhusu mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic ambaye amemaliza mkataba wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV