June 9, 2016


Baada ya kujifua kivyake kwa muda wa takribani wiki mbili, Hassan Kessy sasa ameungana na wenzake na kuonyesha ni kati ya wachezaji wenye kasi waliosajiliwa na Yanga, msimu ujao.

Tayari Kessy ameanza kazi rasmi Yanga ambayo ni timu yake mpya aliyojiunga nayo baada ya mkataba wake na Simba kwisha.

Katika mazoezi hayo, Kessy alionekana ni mwenye kasi na kutimiza kila alichoambiwa na Kocha Hans van der Pluijm, haraka sana.


Beki huyo wa kulia mwenye kasi, amekuwa kati ya wachezaji wa kikosi cha Yanga wanaojifua kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kujiangaa na mechi za kimataifa.

Yanga imefanikiwa kufuzu kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV