June 9, 2016

JUUKO

Kamati ya Usajili ya Simba imeelekeza nguvu katika safu ya ulinzi na inataka beki mmoja wa kati.

Tayari Simba iko katika mazungumzo na mabeki wawili wa kati kwa ajili ya kupata mmoja ambaye ataunda kikosi chake msimu ujao.

“Wameanza mazungumzo na mabeki wawili wa kati, lengo kwanza ni kupata beki mzalendo atakayesaidiana na Juu na Lufunga,” kilieleza chanzo.

“Hao mabeki wawili mmoja timu yake ilifanya vizuri lakini mwingine haikufanya vizuri lakini anaonekana kuwa na uwezo wa juu,” kilifafanua zaidi chanzo.


Pamoja na kuendelea kusaka safu ya ulinzi, lakini safu hiyo ndiyo ilifungwa mabao machache zaidi kwa msimu uliopita ambao Simba ilishika nafasi ya tatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV