June 3, 2016


OMOG
Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon ameingia kwenye rada za klabu ya Simba baada ya kumuweka katika listi ya makocha inaowataka.

Simba imeamua kuachana kabisa na suala la Wazungu na Omog aliyewahi kuinoa Azam FC na kuipa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara kwanza na ya mwisho atakuwa sehemu kati ya wanaotakiwa.

Hata hivyo, inaonekana chaguo la kwanza la Simba ni Kocha Kalisto Pasuwa anayekinoa kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe.

Tayari Salehjembe lilishaandika kuhusiana na Pasuwa ingawa Simba pia inamfuatilia kocha mwingine kutoka nchini Senegal.

“Kweli zoezi limekuwa likifanyika kwa ungalifu mkubwa. Tunahitaji muda na Simba inataka kufanya mambo kwa uhakika. Omog ni sehemu ya ambao wanaweza kupewa nafasi lakini si chaguo la kwanza,” kilieleza chanzo.

Simba imekuwa ikinolewa na Mganda Jackson Mayanja ambaye ni kocha msaidizi.


Hata hivyo, amekuwa ni kaimu kocha mkuu kwa kuwa Simba ilimtimua aliyekuwa Kocha Mkuu, Dylan Kerr raia wa Uingereza siku moja tu baada ya kumwajiri Mayanja ili amsaidie.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV