June 14, 2016


Kocha wa Southampton, Ronald Koeman rasmi ametua kuchukua ujira wa kuinoa Everton.

Kocha huyo raia wa Uholanzi anachukua nafasi iliyoachwa na kocha Roberto Martinez ambaye alionyeshwa mlango wa kutokea baada ya kuwa na msimu unaosuasua.

Koeman amesaini mkataba wa miaka mitatu kuinoa timu hiyo na ataingiza kitita cha pauni million 6, yaani pauni million 2 kila msimu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV