June 29, 2016


Uongozi wa Mtibwa Sugar umesema bado unamhitaji kiungo wake Shiza Kichuya na ikiwezekana, utamshawishi kubaki.

Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser amesema watakaa naye na kuangalia kama inawezekana abaki.

“Tutazungumza naye lakini kikubwa tutaangalia na mchezaji mwenyewe anataka nini.

“Ni kati ya wachezaji muhimu na tunaowahitaji kuendelea kufanya nao kazi,” alisema.

Bayser amekubali kwamba wako katika mazungumzo na Simba lakini bado hawajamalizana kuhusiana na suala hilo.


Tayari kumekuwa na taarifa za Kichuya kukubali kwenda Simba na wanachosubiri ni wao Simba kukubaliana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV