June 24, 2016Bondia Tyson Fury kutoka Uingereza ameumia na hataweza kupigana na mpinzani wake mkubwa Wladimir Klitschko raia wa Ukraine.

Pambano hilo la kuwania ubingwa wa mataji ya WBO, WBA na IBO lilipangwa kupigwa Julai 9 jijini Manchester.

Lakini Fury ameumia akiwa mazoezini na inaelezwa ameteguka mguu wake wakati akikimbia, hivyo hataweza kupigana.

Kwa hali hiyo, Klitschko aliyekuwa amepania kulipa kisasi baada ya kutwangwa, sasa atalazimika kusubiri hadi itakapotangazwa tarehe mpya ya pambano hilo.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV