June 3, 2016Wakati uongozi wa Simba hivi sasa ukiwa katika harakati za kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, mshambuliaji wa Stand United ya Shinyanga, Elias Maguri, ambaye amefunga mabao 15 kwenye msimu huu wa ligi amesema timu hiyo impe mkataba.

Maguri ambaye pia aliwahi kuitumikia Simba msimu wa 2014/15 ameliambia Championi Ijumaa kuwa, yupo tayari kujiunga na timu hiyo kama uongozi huo utataka kumrudisha klabuni hapo.

Alisema soka ndiyo kazi yake hivyo mabaya yote aliyofanyiwa hapo awali klabuni hapo ameshayasahau na yupo tayari kuitumikia klabu hiyo kwa mara nyingine tena.

"Nina mipango mingi sana kwa sasa juu ya soka langu na zaidi ndoto zangu ni kwenda kucheza soka nje ya nchi.

"Hata hivyo, endapo ikijitokeza timu yoyote ya hapa nyumbani nitakuwa tayari kuzungumza nayo na tukifikia makubaliano basi nitajiunga nayo hata kama ni Simba ije tu tuzungumze sina kinyongo na mtu," alisema Maguri aliyewahi kuzichezea Prisons na Ruvu Shooting miaka ya nyuma.

Straika huyo ambaye amemaliza mkataba wa kuitumikia Stand hivi karibuni ni kati ya wachezaji mahiri sana kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.


Maguri alimaliza msimu uliopita akiwa amefunga mabao 15 kwenye Ligi Kuu Bara.

1 COMMENTS:

  1. Kwisha kazi yake,fitna za simba hatari!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV