June 3, 2016


KESSY AKIWA MAZOEZINI
Kocha Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans van Der Pluijm amependekeza jina la beki, Hassan Kessy na kiungo mshambuliaji, Juma Mahadhi liongezwe kwenye usajili wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) yako jijini Cairo nchini Misri.

Hiyo, ni siku chache tangu Kessy asaini kuichezea Yanga akitokea Simba pamoja na Mahadhi aliyetokea Coastal Union wote waliosaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja.

Yanga itawaongeza nyota hao kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Afrika timu inapofika hatua ya makundi ya michuano hiyo inaruhusiwa kuongeza baadhi ya wachezaji.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema, kocha wao ametoa mapendekezo kwa uongozi akiwahitaji wachezaji hao wasajiliwe kwa ajili ya kuwatumia kwenye Kombe la Shirikisho.

Muro alisema, wamewaongeza wachezaji hao kutokana na kanuni za waandaaji Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuwaruhusu na wamefanya hivyo ili kukiongezea nguvu kikosi chao kilichopangwa Kundi A la michuano hiyo.

Aliongeza kuwa, katika usajili wao wa Caf hawatamkata mchezaji kutokana na kupeleka idadi ya wachezaji 24 huku idadi kamili ikiwa ni 30 katika usajili wao.

“Kessy na Mahadhi lazima tuwaongeze kwenye usajili wetu wa Caf, kwa mfano tutawaachaje wachezaji hao kutokana na uwezo wao mkubwa walionao.

“Kocha tayari ametoa mapendekezo ya wachezaji hao kuongezwa katika usajili wa Caf kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chetu kitakachoshiriki hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

“Malengo yetu ni kuchukua ubingwa huo, mwaka huu, hivyo ni lazima tukiimarishe kikosi chetu ili tuweke rekodi Afrika Mashariki Kati,” alisema Muro.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic