June 5, 2016

MANE

Senegal imejihakikishia kucheza Kombe la Mataifa Afrika baada ya kuitwanga Burundi kwa maba0 2-0 ikiwa nyumbani Bujumbura.

Mshambuliaji hatari wa Southampton ya England, Sadio Mane na Biram Diouf ndiyo walioimaliza Burundi kwa kufunga bao moja kila mmoja.

TAMBWE
Ushindi huo unaifanya Senegal kufikisha pointi 15 na kuziacha Burundi na Namibia zikiwa na pointi 6 kila moja katika nafasi ya pili na tatu katika kundi K.

Washambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga na Didier Kavumbagu raia wa Burundi, ambao wameshindwa kuivusha timu yao tokea mechi za awali, nao wataikosa michuano hiyo kama ilivyo kwa wachezaji nyota kutoka Tanzania.


1 COMMENTS:

  1. Hakuna mchezaji achezaye soka la vilaza la bongo awezaye kufanya maajabu nchini mwake.Hao wageni wanaocheza bongo hawana chochote cha Maana bali hubebwa na mfumo wa soka letu la magazetini na kujiona wana viwango kumbe ni vilaza wa kawaida katika soka.Mchezaji mweledi hawezi kuja kucheza soka la bongo,kinachowaleta bongo ni fedha Maana katika ukanda wa Africa mashariki,Tanzania inaongoza kulipa fedha nyingi wachezaji.Kutojitambua kwa wazawa kunawafanya wageni waonekane nyota,kumbe ni nyota zing'aazo katikati ya vijinga vya moto,lakini wanapokutana na wachezaji wa ukweli,unaweza kuwatafuta kwa tochi uwanjani na bado usiwaone.

    Wachezaji wanaocheza soka letu la kizushi bila kujali wanatoka nchi gani,ni wachezaji wa kawaida kabisa.wanaweza kuonekana bora ndani ya CEKAFA tu nje ya hapo unaweza kuwakataa,ni vimeo wa kawaida kabisa.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV