June 5, 2016


Binti wa bondia gwiji, Muhammad Ali aliyefariki dunia leo, ameelezea namna moyo wa baba yake kuendelea kupiga kwa dakika 30 hata baada ya kila kiungo chake kuonekana kimetulia.

Hana Ali, amesema moyo wa baba yake uliendelea kupiga kwa dakika 30 baada ya kila kiungo chake kuacha kufanya kazi.

Binti huyo amesema waliendelea kumkumbatia na kumuombea Kiislamu huku mwisho akisisitiza wana furaha kwa kuwa baba yao amepumzika.

Ali ndiye bondia maarufu kuliko wote waliowahi kutokea katika historia ya ngumi za kulipwa duniani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV