June 5, 2016Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema atarudi mapema zaidi kwa kuwa anahitaji kuanza maandalizi mapema.

Pluijm ambaye yuko mapumzikoni nchini Ghana ambako ndiko anakoishi, amesema anahitaji kuanza maandalizi mapema.

“Mechi za Kombe la Shirikisho zina ugumu, ninahitaji kuanza maandalizi mapema zaidi.

“Huku nilipo, pia kuna maandalizi nimekuwa nikifanya. Kazi itakuwa ngumu,” alisema.


Yanga imefanikiwa kufuzu kucheza hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV