June 12, 2016

MANJI

Yusuf Mehbub Manji amechinda tena kuwa Mwenyekiti wa Yanga kwa kupata kura 1,468 kati ya 1,470 zilizopigwa huku kura mbili tu zimeharibika.

Clement Sanga amerejea katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga ba ya kumgaragaza vibaya mpinzani wake Titus Osoro. Sanga amebeba kura 1,428 kati ya 1,508 zilizopigwa na Osoro akaambulia 80 tu.


Lakini hiyo si ishu kubwa sana kutokana hali ilivyokuwa kwamba wawili hao wangeshinda. Wengi wangependa kujua wajumbe wanane ni akina nani.

Nafasi za ujumbe Wagombea walikuwa 20 na wanane walioshinda kwa mujibu wa katiba ya Yanga ni;
1. Siza Augustino Lymo (1027)
2. Omary Said Amir (1069)
3. Tobias Lingalangala (889)
4. Salum Mkemi (894)
5. Ayoub Nyenzi (889)
6. Samuel Lucumay (818)
7. Hashim Abdallah (727)
8. Hussein Nyika (770)

Ambao wameshindwa na kukosa nafasi ni 
1. David Luhago (582)
2. Godfrey Mheluka (430)
3. Ramadhani Kampira (182)
4. Edgar Chibura (72)
5. Mchafu Chakoma (69)
6. George Manyama (249)
7. Bakari Malima (577)
8. Lameck Nyambaya (655)
9. Beda Tindwa (452)
10. Athumani Kihamia (558)
11. Pascal Lizer (178)

12. Silvester Haule (197)

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV