June 12, 2016


Russia itakutana na rungu la Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) baada ya mashabiki wake kuwashambulia na kuwaumiza wale wa England.

Vurugu kubwa zilitokea wakati wa mechi ya kwanza ya michuano ya Euro 2016 jijini Marseille nchini Ufaransa wakati England na Russia zilipomaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1.

Mashabiki hao walirusha moto na kupiga bunduki za mwangwi zinazotoa moto wa miale, jambo ambalo Uefa inaona si sahihi.

Mashabiki wa England pamoja na kuonekana au kujulikana ni wajeuri, lakini walilazimika kukimbia kutokana na vurugu hizo ambazo awali zilianza hata kabla ya mechi.
2 COMMENTS:

  1. Muosha huoshwa...
    Safi sana Warus...

    ReplyDelete
  2. Yaani pamoja na England kuongoza kwa fujo kumbe ni chamtoto kwa Urusi!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV