June 18, 2016MashabikiI wa Madiba FC juzi Alhamisi walifanya uamuzi mgumu baada ya kuamua kuwaondoa njiwa waliowekwa langoni kwao na wapinzani wao Kauzu FC kwa kuwapiga kama mpira.

Timu hizo zilikutana kwenye Uwanja wa Chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar katika mchezo wa 32 Bora ya Sport Extra Ndondo Cup. Championi Jumamosi lilikuwepo uwanjani hapo ambapo mashabiki hao wa Madiba waliamua kuwapiga njiwa hao wakidai wapo hapo kwa ajili ya mambo ya kishirikina. Mchezo huo uliisha kwa suluhu. 


Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo uliopigwa jana jioni uwanjani hapo ulishuhudia Temeke Market ikipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kinondoni FC ambayo ilijaza wachezaji wengi wa Simba B. Mabao ya Temeke yalifungwa na Uhuru Selemani na lile la wapinzani likifungwa na Vicent Costa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV