June 18, 2016


Ili kuhakikisha inafanya vizuri msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, Ndanda FC imepanga kusajili wachezaji saba kutokana na ripoti ya kocha wao, Malale Hamsini kutaka wafanye hivyo.

 Katibu Mkuu wa Ndanda, Selemani Kachele alisema, wamepanga kuongeza wachezaji saba ili kuimarisha kikosi chao kiweze kupambana ipasavyo.


“Kati ya hao wachezaji saba, mabeki wawili, viungo watatu, straika mmoja na kipa mmoja, tukifanya hivyo tutakuwa fiti zaidi,” alisema Kachele.

Ndanda haikuwa na msimu mzuri sana katika msimu uliopita, na ililazimika kufanya kazi ya ziada ili kubaki Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV