June 26, 2016


Mwanasheria maarufu nchini, Alex Mgongolwa amesema Yanga ndiyo inayopaswa kuwapangia wageni wake wakae sehemu gani kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, keshokutwa.
Mgongolwa amesema, suala la mashabiki wa TP Mazembe wakae wapi, inawahusu Yanga na hawapaswi kuhusika.

“Yanga ndiyo wahusika wakuu, kuhusu mashabiki wa Mazembe, Yanga wanajua wakae wapi na si timu nyingine. 

“Unapozungumzia mechi kama hii, basi Yanga ndiyo wenye maslahi makubwa zaidi. Suala la mashabiki wa Mazembe wenyeji wao Yanga watatoa nafasi na wanajua wakae wapi. Lakini si mashabiki wengine,” alisema Mgongolwa.

Kumekuwa na taarifa kwamba Yanga wanataka kujaza mashabiki wao kila sehemu ya uwanja ili kudhibiti ushangiliaji wa Mazembe.


Lakini kuna taarifa mashabiki wa Simba nao wana mpango kujazana kwa wingi Uwanja wa taifa hiyo keshokutwa kuwaunga mkono TP Mazembe na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeonya kuhusiana na uamuzi huo wa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV