June 4, 2016


Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema anatamani kumtumia nahodha na beki wa kati wa zamani wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ lakini hawezi kumlazimisha baada ya kukataa.

Cannavaro hivi karibuni alitangaza kustaafu kuichezea Taifa Stars ikiwa ni siku chache tangu anyang’anywe cheo cha unahodha na kupewa mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgji, Mbwana Samatta.

Beki huyo baada ya kunyang’anywa cheo hicho haraka alitangaza kustaafu kuichezea Taifa Stars na kubaki na klabu yake ya Yanga iliyotinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.

CANNAVARO
 Mkwasa alisema yeye alikuwa akihitaji uzoefu mkubwa alionao Cannavaro wa kucheza mechi nyingi za ya kimataifa, hivyo anaamini angekuwepo kikosi chake kingeimarika.

“Nilikuwa nahitaji uzoefu wa Cannavaro katika timu, lakini kutokana na yeye mwenyewe kuamua kukataa kujiunga nasi, nimeona nimuache nisiendelee kumlazimisha.

“Mimi sina taarifa za yeye kustaafu na hata hiyo barua aliyosema ameandika haijanifikia, hivyo nimeamua kumuacha, wapo vijana wengine nitakaowatumia,” alisema Mkwasa.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa, akizungumzia hali hiyo, alisema: “Hatujapokea barua ya Cannavaro kustaafu kuichezea Taifa Stars, ndiyo maana aliitwa.”

Lakini Cannavaro alipotafutwa alisema: “Barua nimewapelekea siku nyingi tu na nasisitiza kuwa nimestaafu kuichezea Taifa Stars.”


Mkwasa alimuita Cannavaro ili aichezee Taifa Stars mechi ya leo dhidi ya Misri ya Kundi G kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon), lakini beki huyo amegoma.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV