June 30, 2016Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu Yanga, Jerry Muro amesema baraua aliyotumiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutakiwa kwenda kusikiliza shauri lake, ina mapungufu kibao.

Muro ameiambia SALEHJEMBE kwamba, ameipata barua inayomtaka kwenda kwenye kamati ambako anashitakiwa kuishambulia TFF kwenye vyombo vya habari.

“Lakini hawasemi ni kamati ipi na utaona kuna vitu vingi vina mapungufu sana,” alisema Muro.

Hata hivyo, alikataa katakata kusema atakwenda kwenye shauri hilo au la na kuendelea kusisitiza kwamba kuna mapungufu katika barua hiyo.


Katika mitandao jana yalisambaa maandishi ya Muro akisema kuna fitna anafanyiwa ili afungiwe, kitu anachoamini kimelenga kumziba mdogo ambalo si jambo sahihi.

1 COMMENTS:

  1. muro si mtu wa mpira hata km ana taaluma ya habari lakini suala la soka hajui chochote...anaropoka tu

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV