June 21, 2016


NSAJIGWA
Beki nyota na nahodha wa zamani wa Yanga, Shadrack atamkabidhi kocha Hans van der Pluijm ripoti ya mechi kati ya TP Mazembe dhidi ya Medeama ya Ghana.

Nsajigwa alikuwa mjini Lubumbashi wakati TP Mazembe ikiiangamiza Medeama kwa mabao 3-1 katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Hata hivyo, Nsajigwa hawezi kusema hadharani chochote hadharani kuhusiana na alichoona hadi atakapomkabidhi ubora na udhaifu wa TP Mazembe lakini pia Medeama.

Baada ya kuishuhudia mechi hiyo, Nsajigwa atandaa ratiba na kumtumia Pluijm nchini Uturuki ambako inaendelea na kambi.

Yanga walimpeleka Nsajigwa ili kuishuhudia TP Mazembe ikipambana na Medeama kwa kuwa wao watakuwa dimbani kuwavaa Mazembe Jumanne ijayo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV