June 25, 2016Kiungo wa Juventus, Paul Pogba na Mesut Ozil wa Arsenal wamekuwa wa kwanza kukubali kusaidia kutoa fedha za kusaidia upasuaji wa watoto nchini Tanzania.

Ozil ambaye anaitumikia Ujerumani katika Kombe la Euro 2016 na Pogba ambaye anaitumikia Ufaransa iliyo mwenyeji wa michuano hiyo, wametoa fedha ambazo hazijaelezwa ni kiasi gani kupitia programu ya Big Foot.


Madaktari watawafanyia upasuaji watoto katika eneo la Ifunda mkoani Iringa. Imeelezwa wazazi wao hawakuwa na uwezo wa kifedha kuwawezesha kimatibabu.

Watoto wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji ni 11, wachezaji wataotoa msaada huo ni wale wanaoshiriki michuano ya Euro 2016.

Ozil na Pogba wamekuwa wachezaji wa kwanza kujitokeza, lakini wanatakiwa wachezaji wengine 9 ili kusaidia matibabu ya watoto 11.

Big Foot ilianzishwa mwaka 2006 wakato Togo walipotoa msaada kwa watoto waliokuwa na mattaizo ya afya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV