June 30, 2016


Na Saleh Ally
Aliyekuwa mshambuliaji wa Ndanda FC, Atupele Green ametua JKT Ruvu kwa mkataba wa takribani miaka miwili.

Wakati anasaini rasmi fomu, picha yake inaonyesha mengi ya kuvutia ambayo yanaweza kuwa rekodi mpya ya usajili.

Inaonyesha hivi; 
1. Hakuna meza ya mbwebwe, wanayoitumia ni meza iliyochakaa na imegeuzwa upande droo ndiyo mbele.

2. Atupele anashuhudiwa na watu wanne akisaini fomu hizo, jambo ambalo ni aghalabu kutokea kwingine, mara nyingi ni mtu mmoja au wawili tu, wangetosha.

3. Viti walivyokaa ni vile vya plastiki, tofauti na timu nyingi zingependa kufanya usajili kwenye kiti cha kuzunguka.

4. Eneo unapofanyika usajili, inaonekana si ofisini, haijajulikana ni wapi, huenda ni moja ya maeneo ya jeshi au la.

5. Watu wote isipokuwa wawili, wanaonekana wakiangalia kamera badala ya kushuhudia zoezi la usajili. 


Mwisho unaweza kusema, kazi za jeshi, hakuna kuremba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV