June 19, 2016Kocha Hans van der Pluijm amewaonyesha wachezaji wake kuhusiana na aina ya uchezaji wa kikosi cha Mo Bejaia cha nchini Algeria.

Pluijm raia wa Uholanzi amewataka wachezahi wake kuwa makini na kujilinda na kadi kwa kuwa wachezaji wa Bejaia watalifanya hilo ili kuhakikisha wanapata kadi za njano na ikiwezekana nyekundu.

“Lakini pia nimewasisitiza kwamba wanaweza kufanya kila linalowezekana kuhakikisha tunacheza aina yetu ya uchezaji na si aina wanayoitaka wao, wasitulazimishe kuingia na kucheza wanavyotaka wao,” alisema Pluijm alipozungumza na Cafoline, leo.

Tayari kikosi cha Yanga kimewasili kwenye uwanjani tayari kabisa kwa mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho dhidi ya timu hiyo ya Algeria.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV