June 9, 2016
Yanga iko tayari kwa ajili ya mechi za Kombe la Shirikisho baada ya kutuma majina ya wachezaji wanne.

Hassan Kessy na Juma Mahadhi ni kati ya majina yaliyotumwa na Yanga katika makao makuu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Caf) jijini Cairo, Misri.

Kessy amejiunga na Yanga baada ya mkataba wake na Simba kwisha na Mahadhi ametokea Coasta Union ya Tanga.

Pamoja na hayo, Yanga imeongeza majina mengine mawili ya kiungo wake Andrew Vicent 'Dante' kutoka Mtibwa Sugar na Beno Kakolanya ambaye amejiunga nao akitokea Prisons ya Mbeya.

Awali, Yanga ilipeleka majina 24 Caf, hivyo kuongezeka kwa majina hayo manne, maana yake ni majina 28 na inaendelea kubaki na nafasi mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV