June 20, 2016


Boss kubwa wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Poppe, ametamka kuwa ana uhakika usajili walioufanya na wanaoendelea kuufanya utakirudishia makali kikosi hicho ili kuweza kushindana na wapinzani wao wa jadi, Yanga, ambao waliwafunga katika michezo yote ya msimu uliopita.

Tayari Hans Poppe na viongozi wa Simba wameshafanikiwa kuzipata saini za wachezaji Emmanuel Semwanza na Juma Mnyate (Mwadui), Mzamilu Yassin na Mohammed Ibrahim (Mtibwa Sugar), lakini pia wapo katika mpango wa kushusha maproo sita kutoka nchi mbalimbali.

Hans Poppe alisema kuwa licha ya kuwasajili nyota hao wanne mpaka sasa lakini bado wana mipango thabiti ya kuona wanaendelea kufanya usajili wa wachezaji wenye viwango vya hali ya juu ili msimu ujao wapambane vizuri kwenye michuano watakayoshiriki.

“Kwa namna hii ya usajili ambayo tunaendelea kuufanya, tumedhamiria kuona tunakuwa na kikosi chenye makali katika msimu ujao na tunaamini timu tutakayoiunda itakuwa tishio kwa timu yoyote ile ambayo tutakutana nayo.


“Yaani hata hao Yanga tutakapokutana nao tunataka kuhakikisha tunawafunga kwa sababu kwa msimu uliopita, waliweza kutuonea na kutufunga, hivyo kwa sasa hatutaki kuona jambo hilo linajirudia, pia tunataka kuona furaha inarejea kwetu,” alisema Hans Poppe.

SOURCE: CHAMPIONI  

2 COMMENTS:

  1. Mchawi ndugu,usajili fanya kwa ushirikiano na mwalimu la sivyo unatwanga maji kwenye kinu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic