June 7, 2016Simba imefanikiwa kumbakiza kiungo wake Mzimbabwe, Justuce Majabvi ambaye aliomba kuondoka.

Majabvi alisema anataka kwenda kuishi nchini Australia ambako mkewe amefanikiwa kupata kazi.

Lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema wamekubaliana na Majabvi ataendelea.

“Kweli sasa anabaki baada ya mazungumzo ya mwisho,” alisema Hans Poppe ambaye amekuwa akipambana kuhakikisha Simba inakuwa na kikosi imara msimu ujao.

Hans Poppe alifanya mazungumzo na Majabvi jijini Harare, Zimbabwe kuhusiana na suala hilo. Kabla ya hapo, Majabvi aliwaambia Simba kwamba kuwa kama mwanaye atapata visa ya kwenda kuishi Australia, angeangalia kama kuna uwezekano wa kubaki.


Kama ingeshindikana, mwanaye angebaki Zimbabwe, basi yeye angelazimika kusafiri hadi Zimbabwe na kuishi naye.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV