June 7, 2016


Kikosi cha Yanga kimeanza rasmi mazoezi leo kwa kufanya mazoezi ya kwanza kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Yanga inakuwa timu ya kwanza kuanza mazoezi kabla ya zote kutokana na majukumu yake ya ushiriki wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi.

Yanga imeanza kujifua kwenye Uwanja wa Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam ili kujiweka vizuri kabla ya kuingia kambini.

“Tumefanya mazoezi, yamekwenda vizuri na tutaendelea na programu kesho,” alisema.


Hata hivyo, idadi kubwa ya wachezaji haikuwa imejitokeza badala yake kulikuwa na mchanganyiko wa vijana wa kikosi cha pili ili kupata idadi itakayoonyesha ushindani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV