June 23, 2016


Wakala Mino Raiola ndiye anaonekana kuwa na simu iliyo busy zaidi katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.

Mino raia wa Italia ambaye ni wakala wa kuuza wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) anaonekana kuwa “on fire” kwa kipindi hike kuliko mawakala wengine.

Wachezaji wake ndiyo wamekuwa gumzo la uhamisho huku klabu mbalimbali zikigongana kutaka kuwapata.Baadhi yao ni Zlatan Ibrahimovich anayehusishwa kwenda Manchester United na klabu kadhaa kubwa, pia Paul Pogba ambaye Real Madrid wameishaonyesha nia.


Pia Romelu Lukaku na Mario Balotelli ambaye imeelezwa Mino ameanza mazungumzo na Besiktas ya Uturuki ili ajiunge nayo.

Kiungo staa wa Dortmund, Henrikh Mkhitaryan ambaye anahusishwa na kujiunga na Man United ambayo imelazimika kuongeza dau kumbana, pia yuko chini ya wakala huyo anayeaminika kuwa mjeuri na anayejiamini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV